´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan bin al-Fadhwl bin Bahraan bin ´Abdillaah. Haafidhw, Imaam na mmoja katika wale wanaojulikana.

Abu Muhammad at-Tamiymiy, kisha ad-Daarimiy, as-Samarqandiy. Daarim ni Ibn Maalik bin Handhwalah bin Zayd Manaat bin Tamiym.

Abu Muhammad alizunguka ulimwengu na akatunga vitabu.

Amepokea kutoka kwa Yaziyd bin Haaruun, ´Ubaydullaah bin ´Abdil-Majiyd al-Hanafiy, Wahb bin Jariyr, Muhammad bin Yuusuf al-Firyaabiy, Abu Nu´aym, Abul-Waliyd, Muslim, Khaliyfah bin Khayyaat na wengineo.

Muslim, Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, ´Abd bin Humayd, Muhammad bin Yahyaa, Abu Zur´ah, Abu Haatim na wengineo wamehadithia kutoka kwake.

´Abdus-Swamad bin Sulaymaan al-Balkhiy amesema:

“Nilimuuliza Ahmad bin Hanbal kuhusu Yahyaa al-Himmaaniy Akasema: “Tumemwacha juu ya maneno ya ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan – naye ni imamu.”

Muhammad bin ´Abdillaah bin Numayr amesema:

“´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan ametushinda kwa hifdhi na kumcha Allaah.”

Muhammad al-Mukharraamiy amesema:

“Mwananchi wa Khuraasaan! Muda wa kuwa ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan yuko baina yenu, basi msijishughulishe na mtu mwingine.”

Abu Sa´iyd al-Ashajj amesema:

“´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan ni imamu wetu.”

Muhammad bin Bashshar amesema:

“´Uthmaan bin Abiy Shaybah amesema: “Wahifadhi wa ulimwengu ni wanne, Abu Zur´ah huko Ray, Muslim huko Niysaabuur, ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan huko Samarkand na Muhammad bin Ismaa´iyl huko Bukhaaraa.”

Ibn Abiy Haatim amepokea kutoka kwa baba yake ambaye amesema:

“´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan ndiye imamu wa zama zake.”

Abu Haamid ash-Sharqiy amesema:

“Khuraasaan imezalisha wahifadhi watano; Muhammad bin Yahyaa, Muhammad bin Ismaa´iyl, ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan, Muslim bin al-Hajjaaj na Ibraahiym bin Abiy Twaalib.”

“ad-Daarimiy alikuwa ni katika mabingwa wa kuhifadhi na wenye kumcha Allaah na kujichunga zaidi katika dini ambao wamehifadhi, wakakusanya na wakawa na uelewa katika dini. Ametunga na amehadithia na akaidhihirisha Sunnah nchini mwake, akaita kwayo, akaitetea na kuwaponda wale wenye kwenda kinyume nayo.”

Ishaaq bin Ibraahiym al-Warraaq amsema:

“Nimemsikia ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan akisema: “Alizaliwa mwaka ambao Ibn-ul-Mubaarak alifariki – 181.”

Ahmad bin Sayyaar al-Marwaziy amesema:

“ad-Daarimiy alikuwa na maarifa mazuri na ametunga “al-Musnad” na “at-Tafsiyr.”

Ismaa´iyl bin Ahmad bin Khalaf amesema:

“Tulikuwa kwa Muhammad bin Ismaa´iyl wakati alipoletewa barua ambayo kulikuwa kumeandikwa kwamba ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan amefariki. Akainamisha kichwa chake kisha akasema: “Inna lillaahi wa inna ilayhi Raaji´uun” na machozi yakawa yanatiririka kwenye mashavu yake.

ad-Daarimiy alikuwa nguzo miongoni mwa nguzo za dini. Abu Haatim ar-Raaziy na wengineo wamemfanya kuwa mwaminifu. Bundaar na watu wengine wakubwa wamehadithia kutoka kwake. Tumefikiwa na khabari kwamba Ahmad bin Hanbal alisikia kutajwa kwa ad-Daarimiy ambapo akasema: “Alipewa dunia nzima lakini akaikataa.

Rajaa´ bin Murajja´ amesema:

“Nimemuona Sulaymaan ash-Shaadhakaaniy na Ishaaq bin Raahawayh na jopo la vigogo wengine, lakini sikuwahi kumuona ambaye ni amehifadhi zaidi kama ´Abdullaah bin ´Abdir-Rahmaan.”

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’ (12/224-233)
  • Imechapishwa: 21/09/2020