Ijumaa kwa watu waliosafiri kwenda mashambani

Swali: Nina ndugu wanaoishi kijijini na wamenialika kwenye karamu ya ndoa. Hilo lilikuwa siku ya ijumaa baada ya swalah ya Dhuhr. Nimechanganyikiwa juu ya kwenda kwao kwa sababu ya kutokuwa kwao na msikiti wa kuswalia ijumaa na swalah nyenginezo. Kwa sababu wao ni watu wa shambani na wanaswali nje na hawahudhurii swalah ya ijumaa. Nikaenda kwa ajili ya kuitikia wito kwa sababu ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Mkiitwa basi muitikie.”

Lakini hata hivyo sikuhudhuria swalah ya ijumaa kutokana na sababu iliyotajwa. Je, ninapata dhambi kwa jambo hilo?

Jibu: Ikiwa kwenda kwako kwao ni kabla ya kuingia wakati wa swalah ya ijumaa hakuna neno juu yako. Ikiwa umeenda baada ya kuingia wakati wake, baada ya adhaana ya pili, basi ni haramu kwako. Allaah anasema:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَاةِ مِن يَوْمِ الْجُمُعَةِ فَاسْعَوْا إِلَىٰ ذِكْرِ اللَّـهِ وَذَرُوا الْبَيْعَ

“Enyi walioamini! Inaponadiwa kwa ajili ya swalah siku ya ijumaa, basi kimbilieni kumtaja Allaah na acheni biashara.” (62:09)

Kuna uwezekano pia ukaswali swalah ya ijumaa kisha ukawaendea. Ima ukawaeleza kwamba utawaendea baada ya swalah na ukatoka vivyo hivyo. Ukienda baada ya kuwa wameshamaliza karamu ya chakula utakuwa umeitikia wito. Muhimu ni kwamba haijuzu kwako kuwaendea baada ya kukuwajibikia kuhudhuria ijumaa, hilo linakuwa kwa wito wake. Ama ikiwa kabla ya hapo hakuna neno juu yako na khaswa ikiwa kutoitikia wito wao kutapelekea katika madhara kama ya machukizo na bughudha ya kukata kizazi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (18) http://binothaimeen.net/content/6830
  • Imechapishwa: 13/09/2021