Swali: Mwanamke mwenye wudhuu´ akigusa uchi wa mtoto wudhuu´ wake unatenguka?
Jibu: Wudhuu wa mwanamke hautenguki akimgusa mtoto wake au akagusa dhakari yake au tupu yake. Kwa kuwa hilo halitengui wudhuu´. Hata kule mwanaume akigusa dhakari yake, hakutengui wudhuu´ isipokuwa ikiwa ni kwa matamanio. Ama ikiwa ni bila ya matamanio, imependekezwa kutia wudhuu´ lakini sio wajibu.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Liqaa’ al-Baab al-Maftuuh (09 B)
- Imechapishwa: 14/09/2020