Swali: Ni upi utofauti kati ya Hadiyth-ul-Qudsiy na Hadiyth Nabawiy?
Jibu: Hadiyth-ul-Qudsiy inanasibishwa kwa Allaah (Ta´ala), kwa mfano ”Allaah (Ta´ala) amesema”, lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye anayenukuu kutoka kwa Mola wake. Kwa hiyo huitwa Hadiyth-ul-Qudsiy. Ama isiyoelezwa kutoka kwa Mola wake huitwa Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama maneno yake:
“Hakika si vyengine matendo yanategemea nia.”
”Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano.”
Haya ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Swali: Kwa hiyo ni kwamba maana yake ni kutoka kwa Allaah na tamko lake ni la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?
Jibu: Ni wahy kutoka kwa Allaah, lakini matamshi yake ni ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah amemfunulia maana, kisha Mtume akazieleza kwa maneno yake.
Kuhusu Hadiyth-ul-Qudsiy ni kama maneno ya Allaah (Ta´ala):
”Ee mwana wa Aadam! Kadhalika na kadhalika… Mimi nimeharamisha dhuluma juu ya nafsi Yangu na Nimeifanya kati yenu kuwa haramu. Hivyo basi msidhulumiane. Ee mwana wa Aadam! Nyote mmepotea isipokuwa yule niliyemwongoza. Hivyo basi niombeni uongofu nitakuongozeni…. “
Swali: Je, ina hukumu sawa na Qur-aan?
Jibu: Hapana, ni maneno ya Allaah lakini hayana hukumu ya Qur-aan.
Swali: Je, tamko lake ni kutoka kwa Allaah lakini haikupokelewa kwa mapokezi mengi (متواترًا)?
Jibu: Haina hukumu ya Qur-aan hata kama haikupokelewa kwa mapokezi mengi, haina hukumu sawa na Qur-aan.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31220/ما-الفرق-بين-الحديث-القدسي-والحديث-النبوي
- Imechapishwa: 14/10/2025
Swali: Ni upi utofauti kati ya Hadiyth-ul-Qudsiy na Hadiyth Nabawiy?
Jibu: Hadiyth-ul-Qudsiy inanasibishwa kwa Allaah (Ta´ala), kwa mfano ”Allaah (Ta´ala) amesema”, lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ndiye anayenukuu kutoka kwa Mola wake. Kwa hiyo huitwa Hadiyth-ul-Qudsiy. Ama isiyoelezwa kutoka kwa Mola wake huitwa Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), kama maneno yake:
“Hakika si vyengine matendo yanategemea nia.”
”Uislamu umejengwa juu ya nguzo tano.”
Haya ni maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
Swali: Kwa hiyo ni kwamba maana yake ni kutoka kwa Allaah na tamko lake ni la Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?
Jibu: Ni wahy kutoka kwa Allaah, lakini matamshi yake ni ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Allaah amemfunulia maana, kisha Mtume akazieleza kwa maneno yake.
Kuhusu Hadiyth-ul-Qudsiy ni kama maneno ya Allaah (Ta´ala):
”Ee mwana wa Aadam! Kadhalika na kadhalika… Mimi nimeharamisha dhuluma juu ya nafsi Yangu na Nimeifanya kati yenu kuwa haramu. Hivyo basi msidhulumiane. Ee mwana wa Aadam! Nyote mmepotea isipokuwa yule niliyemwongoza. Hivyo basi niombeni uongofu nitakuongozeni…. ”
Swali: Je, ina hukumu sawa na Qur-aan?
Jibu: Hapana, ni maneno ya Allaah lakini hayana hukumu ya Qur-aan.
Swali: Je, tamko lake ni kutoka kwa Allaah lakini haikupokelewa kwa mapokezi mengi (متواترًا)?
Jibu: Haina hukumu ya Qur-aan hata kama haikupokelewa kwa mapokezi mengi, haina hukumu sawa na Qur-aan.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31220/ما-الفرق-بين-الحديث-القدسي-والحديث-النبوي
Imechapishwa: 14/10/2025
https://firqatunnajia.com/ibn-baaz-kuhusu-tofauti-kati-ya-hadiyth-ul-qudsiy-na-hadiyth-nabawiy/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket