Hukumu ya kuhukumiana kwa hukumu za kimarekani

Swali: Ni ipi hukumu ya kuhukumiana na mahakama ya kimarekani mtu akilazimika kufanya hivo?

Jibu: Mkilazimika kufanya hivo na hamuwezi kupata mali yenu isipokuwa kwa njia hiyo, basi hakuna neno kufanya hivo. Lakini ikiwa mnataka kuhukumiana nayo na wala hamtaki kuhukumiana kwa wanachuoni, basi hiyo ni kufuru. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

أَلَمْ تَرَ إِلَى الَّذِينَ يَزْعُمُونَ أَنَّهُمْ آمَنُواْ بِمَا أُنزِلَ إِلَيْكَ وَمَا أُنزِلَ مِن قَبْلِكَ يُرِيدُونَ أَن يَتَحَاكَمُواْ إِلَى الطَّاغُوتِ وَقَدْ أُمِرُواْ أَن يَكْفُرُواْ بِهِ وَيُرِيدُ الشَّيْطَانُ أَن يُضِلَّهُمْ ضَلاَلاً بَعِيدًا

”Je, huoni wale ambao wanadai kwamba wao wameamini yaliyoteremshwa kwako na yale yaliyoteremshwa kabla yako, wanataka wahukumiane kwa Twaaghuut na hali wameamrishwa wakanushe hiyo, na shaytwaan anataka awapoteze upotofu wa mbali kabisa.” (an-Nisaa´ 04:60)

Kule kutaka kwao kunajulisha nia zao. Unataka kupata haki yako na wala huwezi kuipata isipokuwa kwa njia ya kanuni zilizotungwa na wanadamu,  basi una haki ya kwenda huko. Unataka kuhukumiana kwa kanuni zilizotungwa na wanadamu na wala hutaki kuhukumiana kwa wanachuoni, kuna khatari juu yako ya kukufuru:

أَفَحُكْمَ الْجَاهِلِيَّةِ يَبْغُونَ ۚ وَمَنْ أَحْسَنُ مِنَ اللَّـهِ حُكْمًا لِّقَوْمٍ يُوقِنُونَ

“Je, wanataka hukumu za kipindi cha kijahili? Na nani mbora zaidi kuliko Allaah katika kuhukumu kwa watu wenye yakini.” (al-Maaidah 05:50)

فَلَا وَرَبِّكَ لَا يُؤْمِنُونَ حَتَّىٰ يُحَكِّمُوكَ فِيمَا شَجَرَ بَيْنَهُمْ ثُمَّ لَا يَجِدُوا فِي أَنفُسِهِمْ حَرَجًا مِّمَّا قَضَيْتَ وَيُسَلِّمُوا تَسْلِيمًا

“Naapa kwa Mola wako! Hawatoamini mpaka wakufanye wewe ni hakimu katika yale wanayozozana kati yao kisha wasipate katika nyoyo zao uzito katika yale uliyohukumu na wajisalimishe kwa kujisalimisha.” (an-Nisaa´ 04:65)

وَمَا كَانَ لِمُؤْمِنٍ وَلَا مُؤْمِنَةٍ إِذَا قَضَى اللَّـهُ وَرَسُولُهُ أَمْرًا أَن يَكُونَ لَهُمُ الْخِيَرَةُ مِنْ أَمْرِهِمْ ۗ وَمَن يَعْصِ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ فَقَدْ ضَلَّ ضَلَالًا مُّبِينًا

“Haiwi kwa muumini mwanamme na wala kwa muumini mwanamke pindi Allaah anapohukumu na Mtume Wake jambo lolote iwe wana khiyari katika jambo lao – na yule anayemuasi Allaah na Mtume Wake, basi kwa hakika amepotoka upotofu wa wazi.” (al-Ahzaab 33:36)

Hili ndio jibu. Ikiwa umetenzwa nguvu kwa ajili ya kutaka kupata mali yako na wala hutaki kuhukumiwa kwa Twaaghuut basi hakuna neno. Ama ikiwa unapendelea hukumu zao mbele ya Shari´ah na wakati huohuo una utambuzi juu ya Shari´ah na ukafanya hivo kwa kupenda kwako mwenyewe, basi hiyo inazingatiwa ni kufuru.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.muqbel.net/fatwa.php?fatwa_id=4112
  • Imechapishwa: 21/11/2020