Funga ya Ramadhaan wakati wa mitihani ya masomoni

Swali: Funga ya mwezi huu itakuwa katika masiku ya mitihani na tutashughulishwa zaidi kuliko tulivyokuwa tukishughulishwa hapo kabla. Ni zipi nasaha zako kwa wanafunzi wa kiume na wanafunzi wa kike?

Jibu: Kuhusu wanafunzi wa kike nimesikia kuwa walitanguliza mitihani yao. Kuhusu wanafunzi wa kike nyinyi mnajua kuwa mwanaume ni mwenye nguvu zaidi na mwenye kuweza kustahamili zaidi kuliko mwanamke. Yeye hana shida. Kwenye bega moja unaweza kuweka mfuko wa shayiri na upande mwingine mfuko wa shayiri na hilo likawa si tatizo kwake. Ni mwenye nguvu. Atakuwa – Allaah akitaka – ni mwenye nguvu pia wa kutekeleza mitihani. Lakini kuna jambo linalobaki; ikiwa kila siku kwa mfano ana mazowea ya kusoma juzu tano, siku za mitihani hatoweza. Tunamwambia ni sawa kwani jambo hili ni pana. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kugonjwekwa au akasafiri, basi huandikiwa yale aliyokuwa akiyafanya pindi alikuwa mzima na mkazi.”

Midhali Ramadhaan uliyopita ulikuwa na mazowea ya kusoma juzu tano au juzu kumi na ukashindwa kufanya hivo kwa sababu ya mitihani, basi kunatarajiwa kwamba utaandikiwa thawabu za matendo uliyokuwa ukiyafanya hapo kabla.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1381
  • Imechapishwa: 04/12/2019