Firqat-un-Naajiyah ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah

Swali: Je, kuna tofauti kati ya pote lililookoka (Firqat-un-Naajiyah) na kundi lililonusuriwa (Twaaifat-ul-Mansuurah) au ni hiyo hiyo moja?

Jibu: Ni hiyo hiyo moja. Pote lililookoka ndio kundi lililonusuriwa na wao ndio Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah kama alivyobainisha hilo Abul-´Abbaas (Rahimahu Allaah) kwenye kitabu chake ´Aqiydat-ul-Waasitwiyyah. Amesema:

“Wao ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, pote lililookolewa na kundi lililonusuriwa.”

Ni Maswahabah na wale waliowafuata kwa wema. Vilevile ni wale waliomo juu ya yale aliyokuwemo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah zake. Wao ni pote lililookoka, kundi lililonusuriwa na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Mwenye kutenganisha hayo hana mashiko.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/site/audios/AbdelazizRajhi/Tahauiya2/01.mp3
  • Imechapishwa: 06/09/2020