Damu ya mwanamke ambaye mimba yake imeporomoka katika mwezi wa nne

Swali: Mwanamke mjamzito ana mimba ya mapacha. Mmoja alikufa akiwa tumboni akiwa na miezi mitatu, lakini alitoka tumboni baada ya mwezi wa nne, naye alikuwa hajabaini umbo la binadamu. Yule mwingine akabaki tumboni. Je, damu anayopata mwanamke huyu ni damu ya uzazi au damu ya kawaida?

Jibu: Ikiwa alikwishaumbika, basi hiyo ni damu ya uzazi. Ikiwa ameonekana kuwa na mkono au mguu au kitu cha mfano wa hicho, basi hiyo ni damu ya uzazi. Lakini kama ilikuwa ni damu tu bila kubaini chochote – hakuna mkono, hakuna mguu, hakuna kichwa – basi hiyo ni damu ya kawaida. Katika hali hiyo ataswali, atafunga na atatawadha kwa kila swalah kama hali ya mwanamke mwenye damu ya ugonjwa.

Swali: Kuna kigezo gani cha uumbaji huu?

Jibu: Ni kuwepo kwa dalili zinazoonyesha kipomoko kilichoumbwa, kama kichwa, mkono, mguu au mfano wa hivyo, ndipo itahesabiwa kuwa ni damu ya uzazi.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31072/هل-تكون-نفساء-من-اسقطت-في-الشهر-الرابع
  • Imechapishwa: 30/09/2025