Swali: Kama mke wa baba amegundua kuwa mkwe wake atasafiri pamoja naye nje ya nchi moja kwa moja baada ya kufanya ndoa, je, ni wajibu kwake kumkataza binti yake hilo? Je, ni lazima amtii baba yake na aache kusafiri au amtii mume wake na kusafiri nje ya nchi kwa ajili ya utalii na kustarehe?

Jibu: Baba anaweza kumkataza binti yake kusafiri nje ya nchi na mume wake ikiwa safari hii ni safari ya utalii tu. Mke sio wajibu kwake kumtii mume wake juu ya safari hii. Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumuasi Muumba.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Fataawaa al-Qayyimah lil-Usrah al-Muslimah, uk. 117
  • Imechapishwa: 22/09/2020