Swali: Baba yangu ananitaka mimi kusoma chuo kikuu cha mchanganyiko. Lakini nikakataa. Lakini anatangamana nami kwa ukali tofauti na ndugu zangu wengine kwa sababu ya kukataa kwangu. Unaninasihi nini mimi na yeye?

Jibu: Ni lazima kwa baba kumcha Allaah na arejee katika haki na usawa. Usawa uko pamoja nawe. Ni lazima kwake kurejea katika usawa. Kuhusu wewe usimtii katika kumwasi Allaah:

“Hakuna utiifu kwa kiumbe katika kumwasi Muumba.”

Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema kuhusu wazazi wawili washirikina:

وَإِن جَاهَدَاكَ عَلَىٰ أَن تُشْرِكَ بِي مَا لَيْسَ لَكَ بِهِ عِلْمٌ فَلَا تُطِعْهُمَا ۖ وَصَاحِبْهُمَا فِي الدُّنْيَا مَعْرُوفًا ۖ وَاتَّبِعْ سَبِيلَ مَنْ أَنَابَ إِلَيَّ

“Lakini wakikung´ang´ania kuwa unishirikishe na ambayo huna elimu nayo, basi usiwatii na tangamana nao kwa wema duniani na fuata njia ya anayerudi kutubia Kwangu.”[1]

[1] 31:14-15

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (103) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Ighastah-6-3-1441_1.mp3
  • Imechapishwa: 14/01/2021