Asiyependa matahadharisho juu ya Ahl-ul-Bid´ah na yeye ni katika Ahl-ul-Bid´ah

´Uqbah bin ´Alqamah amesema:

“Nilikuwa nyumbani kwa Artwa´ah bin al-Mundhir pindi mtu mmoja kwenye kikao alisema: “Mnasemaje juu ya mtu mwenye kutangamana na yuko pamoja na Ahl-us-Sunnah, lakini pindi Ahl-ul-Bid´ah wanapokuja anasema: “Tupeni amani na kuwazungumzia. Msiwataje.”? Artwa´ah akasema: “Ni katika wao. Usidanganyike nao.” Sikuridhika na maneno ya Artwa´ah ndipo nikawa nimeenda kwa al-Awzaa´iy ambaye alikuwa ni mjuzi wa mambo haya. Akasema: “Artwa´ah amepatia. Mambo ni kama alivyosema. Yule pale anakataza wasitajwe. Vipi mtu atawaepuka ikiwa hawatajwi?”

  • Mhusika: Imaam ´Aliy bin Thaabit al-Khatwiyb al-Baghdaadiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Taariykh Dimashq (8/15)
  • Imechapishwa: 06/09/2020