Swali: Ni jambo limeenea kwa baadhi ya watu kwamba yule ambaye hana Shaykh basi shaytwaan ndiye Shaykh wake. Unawanasihi nini?

Jibu: Hili ni kosa la upofu na ujinga kutoka kwa baadhi ya Suufiyyah. Lengo ni kuwavutia watu kuungana nao na kuwafuata kichwa mchunga katika Bid´ah na upotofu wao. Kwani mtu akisoma dini kwa kuhudhuria katika ile mizunguko ya kielimu ya kidini au akaizingatia Qur-aan na Sunnah na akafaidika navyo, basi haisemwi kuwa Shaykh wake ni shaytwaan. Bali kunasemwa kuwa amejitahidi katika kusoma elimu na ameifikia kheri kubwa.

Wanafunzi wanatakiwa kuwasiliana na wanachuoni wanaotambulika kuwa na ´Aqiydah na historia nzuri na kuwauliza juu ya yale yanayowatatiza. Kwa sababu akiwa si mwenye kuwauliza wanachuoni basi anaweza kutatizwa na mambo mengi na kubabaishwa na mambo. Ama akihudhuria mizunguko ya kielimu na akasikiliza mawaidha kutoka kwa wanachuoni basi hakika amefikia kheri nyingi na faida kubwa ingawa hana Shaykh maalum. Hapana shaka kwamba ambaye anahudhuria mizunguko ya kielimu, akasikiliza Khutbah za ijumaa, Khutbah za ´iyd na mihadhara inayowekwa misikitini Mashaykh wao ni wengi ingawa hajinasibishi kwa yeyote, akamfuata kibubusa na akamfuata katika maoni yake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/430)
  • Imechapishwa: 22/02/2021