´Aqiydah sahihi pekee inatosha bila ya matendo na kusimama imara?

Swali: Je, ´Aqiydah sahihi inatosha bila matendo na kusimama sawasawa juu ya Shari´ah ya Allaah?

Jibu: ´Aqiydah pekee haitoshi bila ya matendo. Ni lazima kuwe na matendo:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتُ النَّعِيمِ

“Hakika wale walioamini na wakafanya mema watapata mabustaani yenye neema.”[1]

Ni lazima yawepo matendo. Mtu amwamini Allaah, Mtume wake, aamini kuabudiwa kwa Allaah pekee, atekeleze faradhi za Allaah na aache yaliyoharamishwa na Allaah. Ni lazima kuwepo na yote mawili:

إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَهُمْ جَنَّاتُ النَّعِيمِ

“Hakika wale walioamini na wakafanya mema watapata mabustaani yenye neema.”

Hivyo basi ni lazima kuwe na imani na matendo.

[1] 31:08

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30048/هل-تكفي-صحة-المعتقد-عن-الاستقامة-على-الشرع
  • Imechapishwa: 05/09/2025