Anasafiri kwenda katika nchi ambayo mwandamo wao wa Ramadhaan ulichelewa kwa siku kadhaa

Mtu huyu anauliza kwa kusema: alisafiri kutoka Saudi Arabia na kwenda nchi nyingine ambayo ilitofautiana nao katika mwandamo mwezi. Tukadirie kuwa Saudi Arabia mwezi Ramadhaan uliandama usiku wa jumamosi. Hiyo nchi nyingine hawakuanza kufunga isipokuwa usiku wa jumapili. Saudi Arabia wakafunga mwezi mkamilifu na hiyo nchi nyingine [wakafunga mwezi mpungufu]. Hili litapelekea ikiwa atafunga pamoja na watu wa hiyo nchi nyingine basi atafunga siku thelathini na moja. Akila bado kuna utatizi; atakuwa ameacha kufunga na huku watu wamefunga. Nasema – na namuomba Allaah aniwafikishe katika usawa – tukijua kuwa watu hawa ambao wamejichelewesha kuanza na Saudi Arabia wamejichelewesha kwa ukaidi na ili kwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah, basi katika hali hiyo kula hata kama wao wamefunga. Lakini hata hivyo ale kwa kujificha ili asije ni mwenye kutofautiana na wengine waziwazi. Ama tukijua kuwa hilo limetokana na kujitahidi kwao kwa njia ya kwamba hawakuona mwezi na sio kwa sababu ya kutaka kwenda kinyume na Ahl-us-Sunnah, katika hali hii tunamwambia mtu huyu asifungue. Funga pamoja nao japokuwa utakuwa umefunga siku thelathini na moja. Kwa sababu huku ni kujitahidi kwao na Saudi Arabia pia wamejitahidi.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (61) http://binothaimeen.net/content/1386
  • Imechapishwa: 06/12/2019