Ahl-ul-Bid´ah kupingana kwao na maandiko ya Qur-aan na Sunnah    


Wanafalsafa na Ahl-ul-Bid´ah katika Mu´tazilah na wengineo wao wameitanguliza akili mbele juu ya maandiko. Kutanguliza akili mbele ni jambo lililo na athari mbaya: linaonyesha upungufu wa Tawhiyd alionayo mtu. Yule asiyejisalimisha kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) basi Tawhiyd yake inapungua. Kwa sababu hapo itamlazimu kusema kwa maoni na matamanio yake. Kitendo cha kutanguliza akili mbele juu ya maandiko ni miongoni mwa sababu za kuenea kwa ufisadi katika ardhi. Hilo ni vile ufisadi katika ardhi umeingia kupitia mapote matatu:

1- Viongozi madhalimu.

2- Wanachuoni, watawa na wanavyuoni wa wanateolojia wa kiyahudi.

3- Wafanya ´ibaadah waovu ambao wanaabudu kwa ujinga.

Kwanza: Viongozi madhalimu wanapingana na Shari´ah kwa siasa mbovu. Wanaipinga Shari´ah kwa kutumia siasa hiyo na wanaitanguliza mbele juu ya hukumu ya Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

Pili: Wanachuoni waovu ambao wametoka nje ya Shari´ah kwa sababu ya kutumia maoni yao na vipimo vyao vibovu ambavyo kwa vipimo hivyo vinawafanya kuhalalisha ya haramu au kuharamisha ya halali. Watu hawa wametoka katika Shari´ah. Kwa sababu wanatanguliza maoni yao mbele juu ya maandiko ya Qur-aan na Sunnah na wanafanya hivo kutokana na makusudio yenye mapungufu na ambayo ni haribifu.

Tatu: Watawa waovu ambao ni wale Suufiyyah wajinga ambao wanapingana na uhakika wa imani na Shari´ah kwa ladha, ndoto na uvumbuzi wa batili wa Kishaytwaan.

Viongozi madhalimu wanasema siasa ikigongana na Shari´ah basi sisi tunatanguliza siasa mbele. Wanachuoni waovu wanasema akili ikigongana na andiko basi sisi tunatanguliza akili mbele. Watawa waovu na wafanya ´ibaadah waovu wanasema ladha zao na uvumbuzi wao ukigongana na Shari´ah basi tunatanguliza ladha zetu na mambo yetu ya uvumbuzi. Kwa ajili hii ndio maana ´Abdullaah bin al-Mubaarak Imaam ambaye ni mwenye kujulikana:

Kwani dini imeharibika isipokuwa ikiwa ni kutokana na viongozi na watawa na wanateolojia wa kiyahudi ambao ni waovu

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Hidaayah ar-Rabbaaniyyah fiy Sharh al-´Aqiydah at-Twahaawiyyah (01/268-270)
  • Imechapishwa: 23/05/2020