Mtunzi wa kitabu (Rahimahu Allaah) amesema:

Hadiyth nyingine inasema:

“Wamegawanyika mayahudi katika mapote sabini na moja, wakagawanyika manaswara katika mapote sabini na mbili na Ummah wangu utagawanyika mapote sabini na tatu – yote hayo yataingia Motoni ila moja tu.” Maswahabah wakauliza: “Ni lipi hilo, ewe Mtume wa Allaah?” Akasema: “Ni lile litalokuwa katika mfano wa yale niliyomo mimi na Maswahabah zangu.”[1]

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna dalili juu ya kupotea na kupinda kwa mayahudi na manaswara. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Ni lile litalokuwa katika mfano wa yale niliyomo mimi na Maswahabah zangu.”

Nao ni Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah, nao ni kundi lililookoka, nao ni kundi lililonusuriwa. Yote haya ni majina yao. Nao ni Maswahabah, Taabi´uun na wale watakaofuata mfumo wao.

Hii ni habari njema. Ni lazima kubaki kundi lililo juu ya haki ambalo linafuata njia ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na linalofanya mfano wa matendo ya Maswahabah. Haki na ufuataji hautosita katika Ummah huu.

[1] Ibn Maajah (3992), at-Tirmidhiy (2641) na Abu Daawuud (4596). at-Tirmidhiy amesema:

“Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 86
  • Imechapishwa: 21/06/2022