51. ´Aqiydah ya Ibn ´Abdil-Wahhaab juu ya mizani siku ya Qiyaamah

Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Mizani itawekwa na matendo ya waja yatapimwa:

فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ

”Basi ambao mizani yao itakuwa nzito – hao ndio watakaofaulu.”[1]

وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ

“… na yule ambaye mizani [ya matendo] yake [mema] itakuwa khafifu, basi hao ni ambao wamekhasirika nafsi zao; Motoni ni wenye kudumu.”[2]

Madaftari yatatawanywa; wako ambao watapokea madaftari yao kwa mikono yao ya kuume na wako wataopokea madaftari yao kwa mikono ya kushoto.

MAELEZO

Mizani ni mizani ya matendo. Allaah ameitaja ndani ya Qur-aan:

وَالْوَزْنُ يَوْمَئِذٍ الْحَقُّ ۚ فَمَن ثَقُلَتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ َ

“Na mizani siku hiyo itakuwa ni haki. Basi ambao mizani yao itakuwa nzito – hao ndio watakaofaulu.”[3]

وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ

“… na yule ambaye mizani [ya matendo] yake [mema] itakuwa khafifu, basi hao ni ambao wamekhasirika nafsi zao; Motoni ni wenye kudumu.”

وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ  فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ

”Na yule itakayekuwa mizani yake khafifu, basi makazi yake [itakuwa] ni Haawiyah.”[4]

Mizani imethibiti katika Qur-aan. Inahusiana na mizani ya kikweli ilio na masahani mawili. Matendo mema yatawekwa kwenye sahani moja na matendo maovu yatawekwa kwenye sahani jingine. Matendo yake mema yakiwa na uzito atafuzu na kufaulu ufaulu ambao hauna maangamivu baada yake. Matendo yake maovu yakiwa na uzito basi amekula patupu na kukhasirika:

وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُم بِمَا كَانُوا بِآيَاتِنَا يَظْلِمُونَ

”Na ambao mizani yao itakuwa khafifu – basi hao ni wale waliokhasirika nafsi zao kwa yale waliyokuwa wakizifanyia dhulma Aayaat Zetu.”[5]

Katika Aayah zingine:

وَمَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ فَأُولَـٰئِكَ الَّذِينَ خَسِرُوا أَنفُسَهُمْ فِي جَهَنَّمَ خَالِدُونَ

“… na yule ambaye mizani [ya matendo] yake [mema] itakuwa khafifu, basi hao ni ambao wamekhasirika nafsi zao; Motoni ni wenye kudumu.”

وَأَمَّا مَنْ خَفَّتْ مَوَازِينُهُ  فَأُمُّهُ هَاوِيَةٌ

”Na yule itakayekuwa mizani yake khafifu, basi makazi yake [itakuwa] ni Haawiyah.”[6]

Maneno yake:

Wako ambao watapokea madaftari yao kwa mikono yao ya kuume.”

Amesema (Ta´ala):

فَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِيَمِينِهِ فَيَقُولُ هَاؤُمُ اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ

“Ama yule atakayepewa kitabu chake kuliani mwake, atasema: “Hebu chukueni someni kitabu changu!”[7]

Atafurahi na watu watamuona:

اقْرَءُوا كِتَابِيَهْ إِنِّي ظَنَنتُ أَنِّي مُلَاقٍ حِسَابِيَهْ

”… someni kitabu changu! Hakika mimi niliyakinisha kuwa hakiki mimi ni mwenye kukutana na hesabu yangu!”

Bi maana duniani. Nilidhania bi maana nilikuwa na yakini kwamba nitakutana na hesabu yangu na matokeo yake akajiandaa kwa jambo hilo:

فَهُوَ فِي عِيشَةٍ رَّاضِيَةٍ فِي جَنَّةٍ عَالِيَةٍ قُطُوفُهَا دَانِيَةٌ كُلُوا وَاشْرَبُوا هَنِيئًا بِمَا أَسْلَفْتُمْ فِي الْأَيَّامِ الْخَالِيَةِ

”Basi yeye atakuwa katika maisha ya kuridhisha. Kwenye Pepo ya juu. Matunda yake ya kuchumwa ni karibu. [Wataambiwa]: “Kuleni na kunyweni kwa furaha kwa yale mliyoyatanguliza katika siku nyingi zilopita!”[8]

Bi maana yaliyopitika duniani.

وَأَمَّا مَنْ أُوتِيَ كِتَابَهُ بِشِمَالِهِ فَيَقُولُ يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ

“Na ama yule atakayepewa kitabu chake kushotoni mwake, atasema: “Ee, laiti nisingelipewa kitabu changu… “[9]

Huyu atasema laiti nisingeliona daftari hili:

يَا لَيْتَنِي لَمْ أُوتَ كِتَابِيَهْ وَلَمْ أَدْرِ مَا حِسَابِيَهْ يَا لَيْتَهَا كَانَتِ الْقَاضِيَةَ

“Ee, laiti nisingelipewa kitabu changu na wala nisingelijua hesabu yangu! Ee, laiti yangelikuwa mauti ndio kumalizika kwangu!”[10]

Bi maana kifo. Atatamani laiti angelikufa na asije hapo na asifufuliwe:

مَا أَغْنَىٰ عَنِّي مَالِيَهْ

“Haikunifaa mali yangu!”[11]

Duniani:

هَلَكَ عَنِّي سُلْطَانِيَهْ

”Ufalme wangu umeangamia!”

Bi maana hana hoja yoyote mbele ya Allaah (´Azza wa Jall). Kisha Allaah atasema kuwaambia Malaika:

خُذُوهُ فَغُلُّوهُ ثُمَّ الْجَحِيمَ صَلُّوهُ ثُمَّ فِي سِلْسِلَةٍ ذَرْعُهَا سَبْعُونَ ذِرَاعًا فَاسْلُكُوهُ

“Mchukueni na mfungeni pingu kisha kwenye [Moto wa] al-Jahiym mwingizeni aungue. Halafu katika minyororo yenye urefu wa dhiraa sabini mtieni pingu.”

Hii ndio hali miongoni mwa hali za siku ya Qiyaamah iliyotajwa katika Suurah hii. Ni jambo limekariri ndani ya Qur-aan.

[1] 07:08

[2] 23:103

[3] 07:08

[4] 101:06-09

[5] 07:09

[6] 101:06-09

[7] 69:19

[8] 69:21-24

[9] 69:25

[10] 69:25-27

[11] 69:28

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-il-Imaam Mujaddid Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab, uk. 76-77
  • Imechapishwa: 07/04/2021