40. Je, swalah ya kuomba mvua inamlazimu msafiri?

Swali 40: Je, swalah ya kuomba mvua inamlazimu msafiri[1]?

Jibu: Imewekwa kwa watu wa majangwani na wasafiri kuswali swalah ya kuomba mvua wakihitajia jambo hilo. Hilo ni kwa ajili ya kutendea kazi Sunnah za Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Kwa sababu yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiomba mvua wakati wa ukame na akimwomba Allaah (Subhaanah) kuwateremshia mvua waislamu. Kwa hiyo haja ikipelekea wakazi wa jangwani kuomba mvua basi imesuniwa kwao swalah ya kuomba mvua. Vivyo hivyo wasafiri wakihitajia jambo hilo basi imesuniwa kwao kumwomba Mola wao. Allaah (Subhaanah) amesema:

ادْعُونِي أَسْتَجِبْ لَكُمْ

 “Niombeni Nitakuitikieni.”[2]

وَإِذَا سَأَلَكَ عِبَادِي عَنِّي فَإِنِّي قَرِيبٌ ۖ أُجِيبُ دَعْوَةَ الدَّاعِ إِذَا دَعَانِ

“Watakapokuuliza waja Wangu kuhusu Mimi, basi Mimi niko karibu Naitikia du’aa ya muombaji anaponiomba.”[3]

أَمَّن يُجِيبُ الْمُضْطَرَّ إِذَا دَعَاهُ وَيَكْشِفُ السُّوءَ

”Au Yule anayemuitika mwenye dhiki anapomwomba na akamuondoshea uovu?”[4]

Vilevile hapana vibaya wakimwomba msaada Mola wao pasi na kuswali. Kwa sababu imewekwa katika Shari´ah kwa waislamu kumwomba Mola wao haja zao na wajikurubishe Kwake kwa kumtii. Yeye (Subhaanah) ndiye anatakiwa kuombwa na kuulizwa. Yeye ni Mwingi wa kutoa, Mkarimu, Mwingi wa huruma, Mwenye kurehemu. Anatoa kwa hekima na anazuia kwa hekima. Naye juu ya kila jambo ni Muweza. Haulizwi kwa yale Anayoyafanya nao wataulizwa. Lakini kilichowekwa katika Shari´ah kwa waja ni wao kumwomba (Subhaanah) haja zao na wajikurubishe Kwake kwa yale anayoyapenda katika swalah, du´aa, swadaqah na mengineyo.

[1] Majmuu´-ul-Fataawaa (13/66-67).

[2] 40:60

[3] 02:186

[4] 27:62

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ahkaam-ul-Musaafir, uk. 56-57
  • Imechapishwa: 15/05/2022