91 – Ibn ´Abbaas (Radhiya Allaahu ´anhuma) amesimulia: “Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa anaposimama usiku kuswali anasema:
اللهم لك الحمد ، أنت قيم السموات والأرض ومن فيهن ، ولك الحمد لك ملك السموات والأرض ومن فيهن ، ولك الحمد أنت نور السموات والأرض ومن فيهن ، ولك الحمد أنت ملك السموات والأرض ، ولك الحمد أنت الحق ووعدك الحق ولقاؤك حق وقولك حق والجنة حق والنار حق والنبيون حق ومحمد صلى الله عليه وسلم حق والساعة حق اللهم لك أسلمت وبك آمنت وعليك توكلت وإليك أنبت وبك خاصمت وإليك حاكمت ، فاغفر لي ما قدمت وما أخرت وما أسررت وما أعلنت، أنت المقدم وأنت المؤخر، لا إله إلا أنت أو لا إله غيرك
“Ee Allaah! Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye sababu ya kusimama kwa mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye una ufalme wa mbinguni na ardhini na vilivyomo ndani yake. Himdi zote ni Zako. Wewe ndiye nuru ya mbingu na ardhi na vilivyomo ndani yake. Himdi zote ni Zako. Wewe ni Haki. Ahadi yako ni haki. Kukutana na Wewe ni haki. Neno Lako ni haki. Pepo ni haki. Moto ni haki. Mitume ni haki. Muhammad ni haki na Qiyaamah ni haki. Ee Allaah! Kwako nimejisalimisha. Kwako nimetegemea. Wewe nimekuamini. Kwako nimerejea. Kwa ajili Yako nimegombana. Nakuacha uhukumu. Nisamehe dhambi nilizozitanguliza na nilizozichelewesha, nilizozificha na nilizozidhihirisha. Wewe ndiye mwenye kutanguliza na Wewe ndiye mwenye kuchelewesha. Hapana mwabudiwa wa kwa haki isipokuwa Wewe” au ”Hapana mungu mwingine wa haki asiyekuwa Wewe.”[1]
Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.
MAELEZO
Katika Hadiyth hii kuna kufanya Tawassul kwa matendo ya Mola (Subhaanahu wa Ta´ala), kwamba Yeye ndiye Mola wa mbingu na ardhi, kwamba Yeye ndiye amezisimamisha, kwamba Yeye (Subhaanah) ndiye mfalme wa mbingu na ardhi, kwamba Yeye ndiye nuru wa mbingu na ardhi na kwamba kukutana na Allaah ni haki, Pepo ni haki na Moto ni haki.
Ndani yake kuna kumthibitishia sifa zote njema Allaah na kumtegemea Allaah, jambo ambalo ni Tawassul tukufu juu ya matendo ya Allah, usimamizi na sifa Zake na kutambua kuabudiwa Kwake na ule umaalum wa kumwelekea (Subhaanahu wa Ta´ala).
[1] al-Bukhaariy (1120) na Muslim (769).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 94-95
- Imechapishwa: 29/10/2025

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 94-95
Imechapishwa: 29/10/2025
https://firqatunnajia.com/26-duaa-ya-kufungulia-swalah-ya-usiku-ii/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket