Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

160 – Tunathibitisha Pepo juu ya wale kumi ambao walitajwa majina na Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akawaahidi Pepo. Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni ya haki.

161 – Nao ni Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan, ´Aliy, Twalhah, az-Zubayr, Sa´d, Sa´iyd, ´Abdur-Rahmaan bin ´Awf na Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah, ambaye ndiye mwaminifu wa Ummah huu. Allaah awawie radhi wote.

MAELEZO

Hawa kumi ndio ambao wamebashiriwa Pepo. Abu ´Ubaydah (Radhiya Allaah ´anh) amesifiwa kuwa ni mwaminifu wa ummah huu. Wakati Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipoandika mkataba wa amani na Najraan na akawafaradhishia kulipa kodi, amesema Hudhayfah (Radhiya Allaahu ´anh):

“Wakazi wa Najraan walikuja kwa Mtume wa Allaah (Swalla Allahu ´alayhi wa sallam) wakasema: “Tutumie mtu mwaminifu, ee Mtume wa Allaah!” Akasema: “Nitakutumieni mtu mwaminifu kabisa.” Watu wakatazamia hilo. Akamwagiza Abu ´Ubaydah bin al-Jarraah.”[1]

[1]al-Bukhaariy (3745) na Muslim (2420).

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 234
  • Imechapishwa: 27/04/2025