Shaykh-ul-Islaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

3- Yule mwenye kuwaita watu katika kumuabudu.

 MAELEZO

Kama mfano wa wale viongozi wa washirikina ambao wanawaita watu wawaabudu kama mfano wa Fir´awn:

فأَنَا رَبُّكُمُ الْأَعْلَىٰ

“Mimi ni mola wenu mkuu.”[1]

Kama mfano wa Namruud na Suufiyyah waliochupa mpaka ambao huwaita watu kuwaabudu mpaka kiasi cha kwamba wanawausia watu kuwaabudu baada ya kufa kwao ambapo mmoja anawausia wafuasi wake pindi mambo yatawatatiza basi waliendee kaburi lake na wala udongo ulioko kati yake yeye na wao usiwazuie kutokamana naye. Wanawausia watu kuyaendea makaburi yao na wanawaahidi kwamba watawatatulia haja zao. Yule mwenye kuwaita watu wamwabudu wakati yuko hai au baada ya kufa ni miongoni mwa viongozi wa Twawaaghiyt. Kadhalika yule mwenye kuwaita watu kuwaabudu wengine katika Twawaaghiyt ambao ni walinganizi wa shirki. Watu hawa pia ni Twawaaghiyt ambao wanawapambia watu shirki na kuiita kwa mjina yasiyokuwa yake na kwamba kufanya hivo ni katika Tawassul au kwamba ni kwa ajili ya uombezi. Watu aina hii ni wengi. Watu hawa ni Twawaaghiyt kwa sababu wanaita katika shirki. Wanaita katika isiyokuwa ´ibaadah ya Allaah, wanaiita kwa majina yasiyokuwa yake na wanawapambia watu kwa utata na maneno yenye kughuri. Hawa ndio Twawaaghiyt. Walinganizi wa shirki ni Twawaaghiyt. Kila mwenye kuabudiwa badala ya Allaah na wakati huohuo akawa ni mwenye kuridhia jambo hilo, akawaita watu wamwabudu yeye au akawaita watu wamwabudu mtu mwengine asiyekuwa Allaah. Huyu ni katika Twawaaghiyt. Bali ni katika viongozi wa Twawaaghiyt. Tunamuomba Allaah afya.

[1] 79:24

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Thalaathat-il-Usuwl, uk. 302-303
  • Imechapishwa: 24/02/2021