Abu Ja´far at-Twahaawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
102 – Nayo ni maneno ya Allaah (Ta´ala) na hayalingani chochote na maneno ya viumbe.
MAELEZO
Qur-aan ni maneno ya Allaah (Subhaanah) ambayo ameyazungumza kikweli. Jibriyl ameisikia Qur-aan kutoka kwa Allaah kikweli. Baada ya hapo akamfikishia nayo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pasi na kuongeza wala kupunguza:
لَّا يَأْتِيهِ الْبَاطِلُ مِن بَيْنِ يَدَيْهِ وَلَا مِنْ خَلْفِهِ تَنزِيلٌ مِّنْ حَكِيمٍ حَمِيد
“Haiingiliwi na batili mbele na nyuma yake – ni Uteremsho kutoka kwa Mwenye hekima, Mwenye kuhimidiwa.”[1]
وَإِن كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ عَلَيْنَا غَيْرَهُ ۖ وَإِذًا لَّاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًإ إِذًا لَّأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا
”Hakika walikaribia kukukengeusha na yale Tuliyokuletea Wahy ili upate kutuzulia mengineyo. Basi hapo bila shala wangelikufanya rafiki mkubwa. Na lau kama hakukufanya imara, basi hakika ungelikaribia kuelemea kwao kidogo. Hapo bila shaka Tungelikuonjesha adhabu maradufu ya uhai na adhabu maradufu [baada ya] kufa, kisha usingelipata mwenye kunusuru dhidi Yetu.”[2]
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni mwenye kuifikisha Qur-aan bila kupunguza, kuongeza wala kugeuza kitu:
وَلَوْ تَقَوَّلَ عَلَيْنَا بَعْضَ الْأَقَاوِيلِ لَأَخَذْنَا مِنْهُ بِالْيَمِينِ
“Na lau kama angetutungia baadhi za kauli, bila shaka Tungelimchukua kwa mkono wa kuume.”[3]
Qur-aan ni maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala), na imebaki hivyo tangu ilipoteremshwa. Allaah ameihifadhi kuzidishwa na kupunguzwa:
إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ
“Hakika Sisi Tumeteremsha Ukumbusho huu na hakika Sisi bila shaka ndio Tutakaouhifadhi.”[4]
[1]41:42
[2]17:73-75
[3]69:44-46
[4]15:9
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 137
- Imechapishwa: 13/11/2024

Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: at-Ta´liyqaat al-Mukhtaswarah ´alaal-´Aqiydah at-Twahaawiyyah, uk. 137
Imechapishwa: 13/11/2024
https://firqatunnajia.com/127-qur-aan-imehifadhiwa-na-haiwezi-kubadilishwa/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket