11. Katika hali hii mwanafunzi anaishi katika khatari dhidi ya wahalifu

Jambo liko wazi endapo mtu atamwabudu Allaah kwa kumtakasia nia, akawa mkweli katika kujifunza elimu na kuielewa na akajifunza dalili za Kishari´ah hali ya kutaka msaada wa Qur-aan tukufu na Sunnah takasifu, basi Allaah atamsaidia kuzifichua hoja za watu wa batili, kumwondoshea shubuha zao na kumdhihirishia haki. Kunachelea juu yake endapo atapita njia ilihali hana silaha. Kuna khofu juu ya mwanafunzi iwapo atatembea hali ya kuwa hana silaha ya elimu na ujuzi kwa njia ya kwamba akawa anadai elimu lakini pasi na kuielewa na si elimu ya kihakika. Silaha ndio elimu; mtu akanukuu yale yaliyosemwa na Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama akiwa na elimu na uelewa na akamtakasia nia Allaah na akawa mkweli na Allaah, basi Allaah atamsaidia dhidi yao na kumtakasa kutokamana na shari zao. Hakuna ambaye kunachelewa juu yake isipokuwa yule ambaye ima yuko na uchache wa elimu au nia yake imeharibika na hana Ikhlaasw.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-ish-Shubuhaat, uk. 31-32
  • Imechapishwa: 13/10/2021