09. Dhikr inayosemwa wakati wa kushtuka usiku

Fadhilah za ambaye atashtuka usiku

65 – ´Ubaadah bin as-Swaamit (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Mwenye kujigeuzageuza usiku akasema:

لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ، لَهُ الْمُلْكُ وَلَهُ الْحَمْدُ وَهُوَ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ الْحَمْدُ لِلَّهِ، وَسُبْحَانَ اللَّهِ، وَلَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ، وَاللَّهُ أَكْبَرُ، وَلَا حَوْلَ وَلَا قُوَّةَ إِلَّا بِاللَّهِ، ثُمَّ قَالَ : اللَّهُمَّ اغْفِرْ لِي أَوْ دَعَا اسْتُجِيبَ لَهُ، فَإِنْ تَوَضَّأَ وَصَلَّى قُبِلَتْ صَلَاتُهُ

”Hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah, hali ya kuwa yupekee Mmoja asiyekuwa na mshirika, ufalme na himdi zote njema ni Zake, Naye juu ya kila jambo ni muweza. Himdi zote njema ni stahiki ya Allaah, Allaah ametakasika kutokana na mapungufu na hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Allaah ni Mkubwa na hapana uwezo wa kutikisika wala nguvu isipokuwa kwa msaada wa Allaah. Kisha akasema: ”Ee Allaah! Nisamehe” au akaomba du´aa ataitikiwa. Na akitawadha na kuswali itakubaliwa swalah yake.”[1]

 Ameipokea al-Bukhaariy.

MAELEZO

Katika Hadiyth hii kuna fadhilah za mwenye kuamka usingizini ambapo akamtaja Allaah. Ndani yake kuna uwekwaji Shari´ah kwa mtu anapoamka kutoka usingizini kusema Dhikr hii. Ndani yake kuna fadhilah za Dhikr hii na kwamba ni miongoni mwa sababu za kusamehewa, kuitikiwa du´aa na kukubaliwa swalah.

[1] al-Bukhaariy (1154).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Ad´iyah wal-Adhkaar, uk. 74
  • Imechapishwa: 22/10/2025