Kwa kanuni hizi mbili hutatuliwa matatizo mengi: kutofautiana kwa matendo kutokana na tofauti ya uhakika wa imani ndani ya nyoyo, na matendo yanafuta dhambi kulingana na ukamilifu wake au upungufu wake. Kwa hili huondoka mushkila unaowasilishwa na mwenye upungufu wa fungu lake katika mlango huu juu ya Hadiyth inayosema:
“Swawm ya siku ya ´Arafah hufuta miaka miwili na kufunga siku ya ´Aashuuraa hufuta mwaka mmoja.”[1]
Wakahoji kwa kusema kwamba kawaida ya mtu ni kufunga siku ya ´Arafah kila mwaka na akafunga siku ya ´Aashuuraa pia, vipi iwe kufuta miaka mitatu kila mwaka? Baadhi yao wakajibu kwamba kinachozidi baada ya kufuta huinua daraja. Ajabu iliyoje! Laiti mja anapofanya haya yote yenye kufuta dhambi, kwamba yangeliweza kufuta dhambi zake kwa kuungana baadhi yake na baadhi nyingine. Kufuta kwa madhambi haya kunashurutishwa kwa masharti na kunategemea kutokuwepo kwa vizuizi vyote, ndipo hufuta. Ama matendo yaliyozungukwa na ghafla au sehemu yake kubwa na imekosa ikhlaasw ambayo ndiyo roho yake, haikutimizwa haki yake wala haikuthaminiwa kwa thamani yake, basi ni kitu gani kitakachoyafuta haya? Ikiwa mja amejitathmini katika matendo yake kwamba ameitimiza haki yake inavyostahiki kwa dhahiri na ndani na hakuna kizuizi kilichojitokeza cha kuzuia kufutwa kwake, hakuna kitu kinachobatilisha kinachoiharibu, ikiwa ni pamoja na kujikweza, kuona nafsi yake ndani yake, kujifanyia fadhilah kwa hiyo, kutaka kutoka kwa watu wamtukuze kwa hiyo, kutamani moyoni kwake kwa anayemuheshimu kwa hiyo, kumchukia asiyemuheshimu kwa hiyo, kuona kuwa huyo amempunguzia haki yake na kwamba amedharau heshima yake, basi matendo kama haya yatafuta nini? Yale yanayobatilisha matendo na yanayoyaharibu ni mengi kupita kiasi cha kuweza kuhesabiwa. Hivyo basi shani siyo katika matendo, shani iko katika kuyalinda matendo dhidi ya yale yanayoyaharibu na kuyabatilisha. Kujionyesha – hata ikiwa ndogo – huyabatilisha matendo. Kujionyesha kuna milango mingi isiyohesabika. Pia ikiwa matendo hayajafungamanishwa na kufuata Sunnah, hiyo ni sababu ya kuifanya kuwa batili. Pia kujifanyia fadhilah mbele ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) ndani ya moyo wake ni jambo linaloyaharibu matendo. Vivyo hivyo kujifanyia fadhilah kwa kutoa swadaqah, kufanya wema, ihsaan au kuunga jamaa, vyote hivyo vinayaharibu matendo hayo. Kama alivyosmea Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تُبْطِلُوا صَدَقَاتِكُم بِالْمَنِّ وَالْأَذَىٰ
“Enyi mlioamini! Msibatilishe swadaqah zenu kwa masimbulizi na udhia.”[2]
[1] Muslim (1162).
[2] 02:264
- Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 18-20
- Imechapishwa: 29/07/2025

Muhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Abiy Bakr bin Qayyim-il-Jawziyyah (afk. 751)
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Waabil as-Swayyib wa Raafi´-ul-Kalim at-Twayyib, uk. 18-20
Imechapishwa: 29/07/2025
https://firqatunnajia.com/08-una-hakika-kuwa-matendo-yako-mema-yanafuta-madhambi-yako/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket