Ninaiusia nafsi yangu na nyinyi tuzuie ndimi zetu isipokuwa kwa jambo ambalo tunajua wema wake. Tunapowazungumzisha ndugu zetu basi tuwazungumzishe kwa njia iliokuwa nzuri. Allaah (Ta´ala) Amesema:

وَقُل لِّعِبَادِي يَقُولُوا الَّتِي هِيَ أَحْسَنُ

“Waambie waja Wangu waseme ambayo ni mazuri zaidi.” (17:53)

Zuri utaloliona katika matamshi yako basi mzungumzishe nalo baba yako, mama yako, kaka zako, dada zako, mke wako na ndugu zako waumini. Namna hii utafunga njia ya Shaytwaan ambayo ni kuwatenganisha waislamu.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 413
  • Imechapishwa: 13/05/2020