Baadhi ya Salaf wamesema:

“Kuna watu huzungumza sana wao kwa wao. Watu kama hawa kunachelea juu yao kutofanya matendo kwa kuzungumza sana.”

Kuzungumza sana pasina matendo kwa kukaa vikao vya muda mrefu, saa moja, saa mbili mpaka saa tatu kwa maneno yenye kukariri yasiyokuwa na faida, hili ni jambo lenye kulaumika. Lau mtu atazingatia mambo yaliyo ya wajibu ni mengi sana. Utaona baadhi ya watu wanapetuka kwa kufanya mambo yaliyoruhusiwa [mubaah], pengine ndani yake kukaingia maneno na matendo yaliyo ya haramu na huku wameacha mambo mengi yaliyo ya wajibu. Hii sio katika sifa za wanafunzi.

Mwanafunzi matendo yake siku zote yanakuwa kwa yale mambo yaliyo na faida na yeye, bi maana katika yale mambo yenye kumuhusu miongoni mwa yale mambo aliyoamrishwa au kusisitizwa na Shari´ah na aachane na yale mambo yasiyomuhusu katika maneno na matendo, sawa ya dhahiri na ya ndani.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdil-´Aziyz Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh al-Arba´iyn an-Nawawiyyah, uk. 216-217
  • Imechapishwa: 15/05/2020