Swali: Ni sahihi kusema “dini za kimbingu” wakati mtu anakusudia uyahudi, unaswara na Uislamu?

Jibu: Msingi wa dini ya uyahudi na unaswara zinatoka katika Tawraat na Injiyl. Ni vitabu viwili vilivyoteremshwa kutoka kwa Allaah. Kimsingi ni dini za kimbingu. Lakini hata hivyo zimepotoshwa, zimebadilishwa na kugeuzwa. Baadaye zikafutwa kwa Qur-aan tukufu kwa Shari´ah ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini zinaitwa hivo kwa kuzingatia ule msingi wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ma´aalim Manhaj Ahl-is-Sunnah wal-Jamaa´ah, uk. 46
  • Imechapishwa: 29/05/2021