Zichome moto picha ulizohifadhi sasa hivi

Swali: Mimi ni kijana ambaye napenda kuchukua picha na kuhifadhi picha. Hakupitiki mnasaba wowote isipokuwa huchukua picha kwa ajili ya kumbukumbu. Picha hizi nazihifadhi ndani ya albamu. Kunaweza kupita miezi kadhaa kabla sijafungua albamu hii na kutazama picha hizi. Ni ipi hukumu ya picha hizi ambazo nachukua na kuzihifadhi?

Jibu: Ni wajibu kwako kutubia kwa Allaah (´Azza wa Jall) kutokana na ulichokifanya na uzichome moto picha zote ulizohifadhi. Kwa sababu haijuzu kuhifadhi picha kwa ajili ya kumbukumbu. Upesiupesi zichome moto pale tu utaposikia maneno haya.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=CFr4KOOC_oA&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 15/04/2018