Ziada ya mwisho katika adhaana II

Swali: Baada ya kusoma du´aa iliyothibiti baada ya adhaana inajuzu kuzidisha tamko:

إنك لا تخلف الميعاد

“Hakika wewe hauendi kinyume na ahadi Yako”?

Jibu: Hapana, haikuthibiti. Soma mpaka:

آت محمدا الوسيلة والفضيلة وابعثه مقاما محمودا الذي وعدته

“… mpe Muhammad al-Wasiylah na fadhilah mfufue cheo chenye kusifika ambacho umemuahidi.”

Usizidishe na kusema:

إنك لا تخلف الميعاد

“Hakika wewe hauendi kinyume na ahadi Yako”?

kwa kuwa tamko hili halikuthibiti.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (17) http://alfawzan.af.org.sa/node/2110
  • Imechapishwa: 09/07/2020