Ziada mbili dhaifu katika adhaana

Swali 305: Vipi wakati mtu anamuitikia muadhini kusema:

إنك لا تخلف الميعاد

“Hakika wewe hauendi kinyume na ahadi Yako”?

Jibu: Hadiyth hii ya Zayd ndani yake kuna ziada mbili na zote mbili ni dhaifu. Moja ni isemayo:

اللهم رب هذه الدعوة التامة، والصلاة القائمة، آت سيدنا محمد الوسيلة والفضيلة

“Ee Allaah, Mola wa mwito huu uliotimia, swalah iliosimama, mpe bwana wetu Muhammad, Wasiylah na fadhilah… “

Tamko la:

سيدنا محمد

“Bwana wetu Muhammad”

linazingatiwa kuwa ni dhaifu. Aliliongeza at-Twahaawiyyah katika “Sharh al-Maa´niy al-Aathaar”. Linazingatiwa kuwa ni dhaifu. Ziada ya pili pia inazingatiwa kuwa ni dhaifu. Linasema:

إنك لا تخلف الميعاد

“Hakika wewe huendi kinyume na ahadi Yako.”

Muhammad bin ´Awf at-Twaai’ amepwekeka nayo. Wengi wamekwenda kinyume naye. Kwa hiyo tamko hilo linazingatiwa ni dhaifu kama nilivyoyataja hayo katika “ash-Shafaa´ah”. Muhammad bin ´Awf at-Twaai’ amepwekeka nayo. Imaam al-Bayhaqiy ameipokea katika “as-Sunan”. Kwa hiyo ziada mbili hizi ni dhaifu.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 549
  • Imechapishwa: 23/02/2020