Zayd al-Madkhaliy kuhusu Ikhwaaniyyah, Tabliyghiyyah, Qutbiyyah na Suruuriyyah


Swali: Mapote aliyotaja mwandishi – yaani Imaam Ibn Qudaamah katika kitabu chake “Lum´at-ul-I´tiqaad” ametaja Mu´tazilah, Jahmiyyah, Khawaarij, Qadariyyah n.k. – hayaingii katika mapote potevu na makundi ya Bid´ah al-Ikhwaan al-Muslimuun, Jamaa´at-ut-Tabliygh, Qutbiyyah na Suruuriyyah?

Jibu: Ni jambo lisilokuwa na shaka yoyote ya kwamba mapote haya ni katika makundi ya Bid´ah kwa kuwa yameenda kinyume na manhaj ya Salaf katika milango mingi miongoni mwa milango ya elimu na matendo. Wameenda kinyume katika mlango wa I´tiqaad. Baadhi yao wameungana na Suufiyyah kama mfano wa al-Ikhwaan al-Muslimuun, wengi wao, bali viongozi wao wamechanganyika na Suufiyyah, wanasiasa wa sasa na Bid´ah mbali mbali na si kwamba ni Bid´ah moja tu, Bid´ah ya kutoa bay´ah, Bid´ah ya utawala, Bid´ah ya kukusanya [watu kwanza kisha kuwalingania baadaye], kampeni za ugaidi na khaswa katika miji ya Kiislamu, yote haya ni katika sampuli za Bid´ah. Isitoshe wao wako na Ahl-ul-Bid´ah na si kwamba wako katika Ahl-us-Sunnah ambao wanafuata mwenendo wa Salaf.

Tunaposema hivi haina maana tunawatoa katika Uislamu, isipokuwa tu yule ambaye ataleta kauli au ´amali au I´tiqaad inayomtoa katika Uislamu. Hapo ndipo anatoka [katika Uislamu]. Mapote haya ambayo umetaja katika Ikhwaaniyyah, Tabliyghiyyah, Suruuriyyah na Qutbiyyah, wote hawa wako katika mkumbo mmoja na Ahl-ul-Bid´ah na sio pamoja na Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah. Kwa kuwa wanaenda kinyume na manhaj ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah katika mambo mengi. Wasifuatwe na haijuzu kwa yeyote kujiunga nao kamwe. Njia sahihi ni mtu ajaribu kuwa katika manhaj ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah waliotangulia na wa sasa na mtu awe mmoja katika wao. Hii ndio sahihi.

  • Mhusika: ´Allaamah Zayd bin Muhammad al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.njza.net/MultimediaDetails_ar.aspx?ID=960&size=2h&ext=.rm
  • Imechapishwa: 05/09/2020