Swali: Nilifungua akaunti katika benki ya ar-Raajihiy ambapo idara ya wanawake ikanipigia simu na kunipa zawadi ya saa mkabala wa salio. Saa hiyo niifanye nini?

Jibu: Wameona kuwa pesa zake ni nyingi ndio wakasema kuwa anastahiki zawadi hiyo ya saa.

Swali: Nilipokea saa hiyo. Niifanye nini?

Jibu: Salama zaidi na kinachodhihiri ni yeye aiuze na atoe swadaqah pesa atayokuwa amepata. Vinginevyo awarudishie ili wafahamu kuwa kitendo hicho si kizuri.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/21588/حكم-هدايا-البنوك-للعملاء-مقابل-الرصيد
  • Imechapishwa: 29/09/2022