Swali: Wanachuoni wakisema mtu fulani ni zandiki (زنديق) ina maana kuwa ni kafiri?

Jibu: Zandiki kwa mujibu wa istilahi ya waliokuja nyuma ni mnafiki ambao wamezungumziwa na Qur-aan ambao wanadhihirisha imani na wanaficha ukafiri. Huyu ndiye zandiki. Ni yule anayedhihirisha imani na anaficha kumkufuru Allaah (´Azza wa Jall). Huyu huitwa ima mnafiki au zandiki. Yote mawili maana yake ni moja.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (10) http://alfawzan.af.org.sa/node/2053
  • Imechapishwa: 22/01/2017