Zandiki ndiye anayetafuta jawabu lenye kumridhisha

Swali: Nikimuuliza mwanachuoni fulani ambapo akanijibu. Kisha baadaye nikamuuliza mwanchuoni mwingine swali hilohilo. Lengo la kukariri swali hilo ni ili niweze kupata rukhusa. Je, kufanya hivo kuna ubaya? Je, naguswa na maneno ya Salaf:

“Mwenye kufuatafuata rukhusa basi anaingia kwenye uzandiki”?

Jibu: Ndio, katika hali hii kuna ubaya. Umebainisha mwenyewe kwamba unachotafuta ni wewe uruhusiwe. Ni lazima kwako kumuuliza yule ambaye una uaminifu juu ya dini, elimu na kumcha kwake Allaah. Akishakujibu basi itakulazimu kuchukua fatwa yake. Huna khiyari katika jambo hili na wala usimuulize mwengine. Hili ndio jambo la wajibu. Kuhusu kufuatafuata rukhusa ni jambo la haramu kwako.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 09/07/2021