Ni lazima tuwe na inswafu: je, sisi hii leo tuko katika zama za maendeleo au katika zama za uzorotaji? Ndugu! Wakati wa zamani watu wa mashamba, wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), baada ya wakati wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kabla ya jana kulikuwa kunadhaniwa kwamba msichana wa mwanachuoni fulani atatoka amevaa hali ya kuwa bado yuko uchi na eti anakwenda kukamilisha masomo yake Urusi, anaenda kukamilisha masomo yake Uingereza na kwenginepo? Hakika ni jambo ambalo tulikuwa hata hatulifikirii. Je, katika kipindi kile alikuweko muislamu anayeipiga vita dini ya Allaah? Hakuweko. Walikuwa wanapotolewa mawaidha basi hulia. Hawakuwa wanampachika majina bandia kwamba ni Wahhaabiy, kibaraka wa Saudi Arabia, kibaraka wa Marekani au kwamba ni baraka wa fulani na fulani. Hii leo kwa sababu ya shubuha zinazotolewa na maadui wa Uislamu mlinganizi anayelingania kwa Allaah amekuwa ni mwenye kutuhumiwa tuhuma aina mbalimbali.

  • Mhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Ijaabatu as-Saa-il, uk. 302
  • Imechapishwa: 28/09/2019