Zakaat-ul-Fitwr ya mwenye kusilimu kwa mujibu wa Maalik

Maalik amesema:

“Mwenye kusilimu ambaye ameingia katika Uislamu baada ya kuchomoza kwa jua siku ya Fitwr inapendeza kwake kutoa Zakaat-ul-Fitwr.”

Amesema:

“Kuhusiana na Udhhiyyah, naonelea kuwa dhahiri zaidi kwamba analazimika kuchinja.”

Maalik amesem:

“Kipomoko tumboni hakitolewi Zakaat-ul-Fitwr. Lakini mama akijifungua siku ya Fitwr au usiku wa kuamkia siku ya Fitwr, basi ni lazima kumtolea Zakaat-ul-Fitwr mtoto huyu mchanga.”

  • Mhusika: Imaam Sahnuun bin Sa´iyd at-Tanuukhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mudawwanah al-Kubraa (1/114)
  • Imechapishwa: 01/05/2022