Zakaat-ul-Fitwr ya mtoto kwa wazazi kwa mujibu wa Maalik

Ibn-ul-Qaasim amesema:

“Maalik amesema kuwa mtu ambaye analazimika kuwahudumia wazazi wake basi anatakiwa kuwatolea Zakaat-ul-Fitwr.”

Tulimuuliza Maalik kuhusu mtoto ambaye anahitaji kuwasaidia wazazi wake kwa sababu wanamuhitaji; je, ni lazima awatolee Zakaat-ul-Fitwr? Akajibu ndio.

  • Mhusika: Imaam Sahnuun bin Sa´iyd at-Tanuukhiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Mudawwanah al-Kubraa (1/116)
  • Imechapishwa: 01/05/2022