Zakaat-ul-Fitwr kwa mtoto na kipomoko


Swali: Je, mtoto ambaye hakufunga atolewe Zakaat-ul-Fitwr pamoja na kipomoko kilichomo tumboni?

Jibu: Kuhusu mtoto Ibn ´Umar ameeleza:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Zakaat-ul-Fitwr pishi ya tende au pishi ya ngano kwa mvulana na msichana, mdogo na mkubwa, muungwana na mtumwa katika waislamu.” al-Bukhaariy (1503) na Muslim (984).

Kwa hivyo mtoto anatakiwa kutolewa Zakaat-ul-Fitwr kwa sababu ni haki ya waislamu.

Kuhusu kipokomo kilichomo tumboni, ´Uthmaan bin ´Affaan amependekeza mtu kukitolea.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalush-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://af.org.sa/en/node/4270
  • Imechapishwa: 23/06/2017