Swali: Kuna mtu amejitolea Zakaat-ul-Fitwr yeye mwenyewe na familia yake. Kisha akamtolea dada wa mke wake na mvulana wake. Dada wa mke ni muweza wa kujitolea zakaah yeye mwenyewe. Nikamwambia kwamba yeye ajitolee mwenyewe ambapo baadaye akanipa kiwango kilekile nilichomtolea yeye na mvulana wake. Je, inatosha?

Jibu: Midhali amemtolea kwa idhini yake, lengo limefikiwa. Hakuna haja ya mlolongo wote huu. Inajuzu kumlipia mwengine, jambo ambalo limetokea katika hali hii. Hakuna haja ya mlolongo wote huu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (12) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/umdah%20Fiqh-19-10-1434_0.mp3
  • Imechapishwa: 17/09/2017