Zakaah ya pesa ambayo mtu amekopesha

Swali: Kabla ya zaidi ya mwaka mmoja kuna mtu alikopa pesa kutoka kwangu. Bado hajalipa mpaka sasa. Je, nitoe zakaah kwa hizo pesa zilizoko kwake?

Jibu: Ikiwa una uhakika kuwa atakurudishia nazo, basi uzitoe zakaah kila mwaka. Ama ikiwa huna uhakika kama atakurudishia kutokana na hali yake ngumu au anachelewesha kulipa kwa kukusudia, hizi huwezi kuzitoa zakaah mpaka pale utapozipokea mkononi. Utapozipokea mkononi zitoe zakaah kwa ajili ya mwaka mmoja tu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (62) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/Fathul%20Majd14-07-%201438.mp3
  • Imechapishwa: 06/08/2017