Swali: Mimi nina bustani linalotoa matunda kila mwaka. Je, nitoe zakaah juu ya matunda yanatoka katika bustani hili?

Jibu: Matunda hayana zakaah. Zakaah itatolewa juu ya kile kima/thamani yake. Ukiyauza na pesa zikatimiza mwaka mmoja (النصاب), hapo ndipo utatakiwa kulipa zakaah. Ama kuhusu matunda yenyewe hayana zakaah. Zakaah inakuwa katika nafaka na mazalisho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (6) http://alfawzan.af.org.sa/node/14379
  • Imechapishwa: 05/12/2016