Zakaah ni miongoni mwa amri za Mola aliwaamuru Mitume Yake mwa mujibu wa Biblia

30Zaka za mazao iwe ni nafaka au matunda ya miti, yote ni mali ya Mwenyezi Mungu; ni takatifu kwa Mwenyezi Mungu. 31Kama mtu akitaka kuikomboa zaka yake, atalipa thamani yake na kuongeza asilimia ishirini ya thamani ya zaka hiyo. 32Kuhusu mifugo, inapohesabiwa, kila mnyama wa kumi ni mtakatifu kwa Mwenyezi Mungu. 33Mtu yeyote hana ruhusa kuuliza kama mnyama huyo ni mzuri au mbaya wala mnyama huyo kamwe hatabadilishwa kwa mwingine. Kama akibadilishwa kwa mwingine, wanyama wote wawili watakuwa watakatifu; hawatakombolewa.” 34Hizo ndizo amri ambazo Mwenyezi Mungu alimwamuru Mose ili awaambie waisraeli, mlimani Sinai.

  • Marejeo: Walawi 27:30-34
  • Imechapishwa: 02/02/2020