Zakaah mke kumpa mume


Swali: Inajuzu kwangu kupokea zakaah ya dhahabu kutoka kwa mke wangu pamoja na kuzingatia kwamba yeye ni mwalimu na mimi mpaka hivi sasa sifanyi kazi?

Jibu: Inajuzu kwa mwanamke kumpa zakaah yake mume wake ikiwa ni miongoni mwa wale watu wanaostahiki kupokea zakaah. Ni mamoja zakaah hiyo ni ya dhahabu au zakaah ya mali. Hivo ni kwa sababu mke halazimiki kumhudumia mume mpaka tuseme kuwa ikiwa atampa zakaah mume basi atakuwa ameiokoa mali yake. Hivyo inafaa kwa mke kumpa zakaah ya mali mume wake akiwa ni katika wale wanaostahiki kupewa zakaah.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (71) http://binothaimeen.net/content/1629
  • Imechapishwa: 25/03/2020