Zakaah kwa ajili ya kununua misahafu


Swali: Mimi nina pesa ya zakaah. Je, inajuzu kwangu kununua misahafu na kuitawanya misikitini?

Jibu: Hapana. Zakaah hainunuliwi misahafu. Inatawanywa kwa mafukara na wengineo:

إِنَّمَا الصَّدَقَاتُ لِلْفُقَرَاءِ وَالْمَسَاكِينِ وَالْعَامِلِينَ عَلَيْهَا وَالْمُؤَلَّفَةِ قُلُوبُهُمْ وَفِي الرِّقَابِ وَالْغَارِمِينَ وَفِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَابْنِ السَّبِيلِ ۖ فَرِيضَةً مِّنَ اللَّـهِ ۗ وَاللَّـهُ عَلِيمٌ حَكِيمٌ

“Hakika zakaah ni kwa ajili ya mafakiri na masikini na wanaozitumikia na wanaotiwa nguvu nyoyo zao na kuwakomboa mateka na wenye deni na katika njia ya Allaah na msafiri; ni faradhi inayotoka kwa Allaah. Na Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye hekima.” (09:60)

Ni watu aina nane.  Zakaah hainunuliwi misahafu wala nyumba. Inapewa mafukara na masikini na wale wengine waliotajwa na Allaah. Hazijengewi masomo wala miradi mingine.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (86) http://alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/NEW.lite_.mp3
  • Imechapishwa: 14/10/2018