Zakaah kuwapa jamaa ndugu


577- Nilimsikia Ahmad akiulizwa kuhusu mtu ambaye anatoa zakaah yake kuwapa jamaa ndugu zake. Akajibu:

“Ikiwa watu wengine ndio wenye kuhitajia zaidi na anachotaka yeye ni kuwatajirisha jamaa ndugu zake na kuwaacha wengine, basi asifanye hivo.”

Aliulizwa vipi ikiwa jamaa ndugu hao ni mafukara kama wengine. Akajibu:

“Kama mambo ni hivo basi wao wana haki zaidi ya kupewa zakaah.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 119
  • Imechapishwa: 26/02/2021