Zakaah kumpa mke na kaka na dada


576- Nilimsikia Ahmad akisema:

“Mume asimpe zakaah mke wake.”

Nilimuuliza swali hilo mara nyingi na kila mara hunipa jibu kama hilo.

Aliulizwa kuhusu zakaah kuwapa ndugu kaka na dada ambapo akajibu:

“Hakuna neno ikiwa lengo la kufanya hivo sio kukinga kitu au kuondosha kitu kibaya.”

  • Mhusika: Imaam Abu Daawuud Sulaymaan bin al-Ash´ath as-Sijistaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad, uk. 119
  • Imechapishwa: 27/02/2021