Zakaah juu ya sanduku ambalo familia wanachanga pesa

Swali: Kipindi cha mwisho familia nyingi zimekuwa zikitenga sanduku maalum kwa njia ya kwamba yule mwanafamilia ambaye anahitajia pesa anakopa kutoka hapo kwa ajili ya lengo lolote. Je, sanduku hilo linahitajia kutolewa zakaah?

Jibu: Ikiwa wale wanaoweka pesa zao ndani ya sanduku hili wanaamini kwamba umiliki wao ni wenye kubaki juu ya hiki walichoweka kwa ajili yake…. kwa maana nyingine iwapo atataka kuzichukua anaweza kuzichukua na kwamba endapo atakufa atarithiwa kwazo, katika hali hiyo umiliki ni umiliki wa watu wote na hivyo zakaah itakuwa ni lazima. Zindukeni juu ya maelezo yangu ili kusiwe na utatizi wowote.

Ama ikiwa yule anayechangia pesa katika sanduku hili anaamini kuwa pesa hizi ni zenye kutoka nye ya umiliki wake, hana uwezo wa kuzichukua tena na hatorithiwa baada yake, pesa hizi hazina zakaah. Kwa sababu ni zenye kutoka nje ya umiliki wake.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (68) http://binothaimeen.net/content/1529
  • Imechapishwa: 15/02/2020