Zaidi ya miaka ishirini na tano haoshi kichwa anapooga janaba

Swali: Kuna mwanamke ameolewa sasa ni zaidi ya miaka ishirini na tano. Mwanzoni mwa kuolewa kwake pindi anapooga janaba basi anaosha mwili wake isipokuwa kichwa chake tu kwa sababu ya ujinga wa kutolijua hilo. Mume wake akamweleza hukumu. Ni ipi hukumu ya zile swalah alizoswali pamoja na kuzingatia ya kwamba mambo haya aliyafanya kwa muda mrefu na hajui ni muda kiasi gani alifanya hivi?

Jibu: Ikiwa haikumpitikia kichwani mwake kwamba kuosha kichwa ni wajibu wakati wa kuoga janaba na wala hakuna aliyemtajia hilo, basi nataraji kwamba haitomlazimu kuzirudi. Ama ikiwa ilimpitikia kichwani mwake lakini hata hivyo akazembea na akapuuzia, basi ni wajibu wake kuzirudi. Atazirudi vipi? Anatakiwa kuzikadiria na kuchukua lile la usalama zaidi. Kile ambacho atakuwa nacho dhana yenye nguvu basi hicho ndicho atacholipa na kila ambacho hatokuwa nacho dhana yenye nguvu hatokilipa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1238
  • Imechapishwa: 18/09/2019