Zabibu kavu kabla ya zabibu zilizokomaa

Nakaribia kutositisha kushangazwa na ndugu yetu muheshimiwa Shaykh Muqbil bin Haadiy. Ni vipi anaweza kuwahimiza huyu na mfano wake – kama mfano wa al-´Adawiy na al-Mu´adhdhin – kutumbukia katika mtego wa kukosoa katika elimu hii? Bado ni wachipukizi. Kwa nini wananishughulisha kuitumikia Sunnah kwa mimi kuwaraddi, ijapo inahusiana na muda kidogo tu? Hanufaiki kitu kwa kuandika katika utangulizi:

“Ndugu yetu ´Aadiyl, ingawa hayuko katika ngazi moja na Muhaddith wa leo Shaykh Muhammad Naaswir-ud-Diyn… “

Ni haki kabisa, lakini mimi siko katika ngazi hiyo iliyotajwa. Hata hivyo naona kuwa ni wajibu wa Shaykh kuwanashi chipukizi hawa kuisoma elimu hii mpaka wakomae kwanza. Halafu wawanufaishe Ummah kwa kueneza  masomo ya Hadiyth na Fiqh ambayo wanaona kuwa watu wanayahitajia, ili watu waweze kupata matunda ya elimu yao na waishuhudilie. Hivi kwani watu hawa hawatambui kuwa wakijishughulisha kumraddi yule ambaye kunadaiwa kuwa eti ni `Muhaddith wa zama hizi` basi atalazimika kuwaraddi na kufichukua aibu na ujinga wao? Hawatambui kuwa wamekuwa zabibu kavu kabla ya kuwa zabibu zilizokomaa?

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/1/386-387)
  • Imechapishwa: 01/08/2020